Bodi ya Korosho Tanzania imeipatia Halmashauri ya wilaya Kilindi kilo 1000 za mbegu ya Korosho ili zigawanywe kwa wakulima kwa lengo la kuinua kipato cha kaya na Taifa
Mratibu wa zao la Korosho katika Halmashauri ya wilaya Kilindi bwana Paul Ntukwe alisema jumla ya ekari 34,000 katika kata 19 zinalimwa Korosho
Alisema Bodi ya Korosho katika awamu mbili imeshatoa dawa za Sulphur ya unga na dawa ya Ukungu na sumu za wadudu na kuongeza kuwa kadri siku zinavyozidi kwenda wakulima wa Korosho wanaongezeka katika Wilaya
Alisema sanjari na hayo Bodi ya Korosho imekuwa ikwapatia wakulima vitu vingine kwa bei za Ruzuku ikiwemo Mabomba ya kupulizia dawa ambayo dukanI huuzwa kwa shilingi laki 7 lakini kwa bei ya ruzuku bomba hilo linauzwa shilingi 350,000/
Bwana Ntuku aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa serikali kuwapatia maafisa ugani vyombo vya usafiri ili kurahisisha kazi zao haswa katika kuwatembelea wakulima na kutoa elimu ya masuala mbalmbali ya kilimo bora chenye tija.
Modi Mngumi
MWISHO
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.