Halmashauri ya wilaya Kilindi yajiandaa kuanzisha kitengo cha matibabu ya utapiamlo mkali kitachosaidia wakazi wake kupata matibabu mahali walipo badala ya kufuata matibabu hayo katika hospitali ya mkoa Bombo
Akitoa maelezo ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha robo ya kuanzia Januari hadi Machi 2023 Mratibu wa kitengo cha lishe ndugu Philimon Nsodya Alisema tayari wataalam sita wakiwemo wataalam wa lishe 2,wauguzi 2 na madaktari 2 wameshapatiwa mafunzo katika hospitali ya Bombo namna ya kuhudumia na kutibu wagonjwa wa utapiamlo mkali
Alisema kitengo cha lishe tayari kimeshafanikisha kupatikana kwa vitepe vya kupimia mzunguko wa mkono(MUAC Tapes) kwa ajili ya kupimia watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kubaini watoto walio na tatizo la utapiamlo
Nsodya alisema vitepe hivyo vimepatikana kutoka ofisi ya Afisa lishe mkoa baada ya kuona uhitaji na kukosekana kwa mzabuni na kuongeza kuwa zoezi la upimaji litaanza mwezi Juni 2023 kama mwezi wa Afya
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa wilaya Kilindi Mh:Abel Busalama aliwataka maafisa tarafa,kata na vijiji kushirikiana na watoa huduma ngazi ya jamii kuelimisha jamii kuwa utapiamlo mkali unatibika na kinachotakiwa ni kuwahi katika vituo vya huduma za afya mara anapoonekana mtoto au mtu mzima ana tatizo la utapiamlo
Modi Mngumi
Mawasiliano Serikalini Kilindi Halmashauri ya wilaya Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.