Halmashauri ya wilaya Kilindi imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 296.6 kwa vikundi vya vijana,wanawake na walemavu.
Mikopo hiyo imekabidhiwa kwa vikundi hivyo baada ya kukidhi vigezo vya kukopeshwa ili kuwajengea uwezo wanawake,vijana na walemavu kujikwamua kiuchumi
Hafla ya uzinduzi wa miradi ya vikundi hivyo ilifanyika katika makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya Kilindi Mh:Abel Busalama na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali na watumishi wa Halmashauri.
Akizungumzia mikopo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi ndugu Gracian Makota alisema Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani itaendelea kuviwezesha vikundi vya vijana,wanawake na walemavu kuvipatia mikopo na mafunzo ya namna ya kuendesha miradi yao
Naye mgeni rasmi akiongea katika hafla hiyo aliipongeza Halmashauri kwa kutoa mikopo hiyo ambayo itaviwezesha vikundi vilivyopatiwa mikopo kuboresha miradi yao na hatimaye kuinua kipato cha kaya na taifa.
Miaradi iliyopatiwa mikopo ni ununuzi wa Bodaboda 38,mashine 10 za kiwanda kidogo cha kufumia masweta,Bajaji 4 na Guta 1,mashine ya kukaushia iliki,mashine ya kusaga na kukoboa,kilimo,ufugaji na kununua vifaa kwa ajili ya kuanzisha Bakery ya mikate
Modi Mngumi-Kilindi
MWISHO
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.