Bodi ya Pamba imeipatia tena Halmashauri ya wilaya Kilindi tani 5 sawa na kilo 5000 za mbegu ya Pamba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi bwana Gracian Makota alisema Halmashauri imeongezwa mbegu hizi baada ya kufanya vizuri katika kuhamasisha wakuma kulima zao hilo katika kata 5
Alisema nyongeza ya mbegu hii ni itagawanywa katika kata 3 zilizoonyesha hamasa kubwa zaidi ambazo ni Negero tani 1.8,Jaila tani 1.6 na Msanja tani 1.6
Alisema Halmashauri ya wilaya Kilindi katika awamu ya kwanza imepokea mbegu za pamba tani 3.25 sawa na kilo 3250 na kuzisambaza katika kata 5 ambazo ni Mabalnga,Msanja,Jaila,Mkindi na Negero ambapo kila kata ilipata kilo 650
Mkurugenzi Makota alisema uzinduzi wa kuhamasisha wananchi wa wilaya Kilindi kulima zao la Pamba ulifanyika mwezi wa Februari 2023,katika kitongoji cha Tilwe,kijiji cha Muungano kilichopo kata ya Msanja ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huu alikuwa mkuu wa wilaya Kilindi Mh Abel Busalama
Alieleza zaidi kuwa hadi sasa Halmashauri katika awamu zote mbili imepokea jumla ya tani 8.25 zinazotosha kupanda ekari 825 za pamba katika msimu huu wa kilimo.
Alisema Uongozi wa Halmashauri ya wilaya Kilindi unatoa shukrani kwa serikali inayoongozwa na Mh Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuinua uchumi wa wakulima katika Halmashauri.
Zao la pamba litasaidia wakulima kuinua kipato chao na halmashauri kuongeza mapato.
Zao la pamba pia litasaidia wakulima kuhifadhi chakula kwani wakulima wengi hutegemea mahindi na aharagwe kama zao la chakula na biashara.
Modi Mngumi
Kitengo cha mawasiliano serikalini
Halmashauri ya wilaya Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.