MAELEZO BINAFSI
Mkurugenzi Mtendaji anaepigania matokeo chanya, mhamasishaji wa shughuli za maendeleo aliye na uwezo wa kuendeleza na kuimarisha timu ya usimamizi ya wataalamu wa Halmashauri ili kuiongezea Halmashauri faida na ufanisi katika huduma zake inazotoa.
Mwenye uzoefu wa kukuza na kuendeleza sekta ya umma ili iwe na nguvu kwa maslahi mapana ya Halmashauri.
UZOEFU WA KAZI
Halmashauri ya wilaya ya Kilindi
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya: Julai 2016 hadi sasa
Kubuni, kukuza na kuendeleza mikakati mbalimbali ya Halmashauri kwa wakati, ufanisi na gharama nafuu.
Msimamizi wa shughuli za kilasiku za Halmashauri, ikiwa ni pamoja na kuongoza vikao, kusimamia watumishi na mipango ya maendeleo kwa kushirikiana na wataalamu wa Halmashauri.
Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa
Mkuu wa Idara - Ardhi na Maliasili : Julai 2007 - Julai 2016
Kuratibu na kudhibiti uendelezaji wa Miji na Vijiji.
Kuratibu uandaaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi Vijijini na Mijini.
Kujenga uwezo wa kupanga na kutekeleza majukumu ya uendelezaji ardhi kwenye Halmashauri.
Kuelimisha jamii kuhusu Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi.
SIFA ZA KITAALUMA
Shahada ya uzamili ya Sayansi katika Usimamizi wa Maliasili na Kilimo Endelevu (MSc. MNRSA)
Chuo Kikuu cha Sokoine
Shahada ya Sayansi katika Mipango Miji na Mikoa (B.Sc. URP)
Chuo Kikuu cha Ardhi
UANACHAMA
Registered Town Planner
Tanzania Association for Town Planners
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.