Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani katika kusheherekea Sherehe za Eid ametoa Mchele Kg. 50, Sabuni, Unga, Mafuta ya kupikia, Mbuzi mmoja na Sukari kwaajili ya sikukuu ya Eid katika kituo cha kulelea Watoto waliokatika Mazingira magumu cha Antonio Kilichopo kata ya Kwediboma Wilaya ya Kilindi.siku ya tarehe 10/04/2024.
Kituo cha Antonio kilichopo chini ya Masister wa Kanisa Katoriki ni Miongoni mwa Vituo vya kulelea Watoto waishio katika mazingira magumu Wilayani Kilindi.
Akikabidhi zawadi hizo kutoka kwa Mheshimiwa Rais, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Hashimu Mgandilwa alisema “ Rais anatamani sana kushiriki sherehe hii na watoto wote wanaoishi katika mazingiara magumu lakini kutokana na Majukumu aliyonayo imekuwa vigumu hivyo amenituma niwaketee zawadi hizi”
Wilaya ya Kilindi ni miongoni mwa Wilaya ambazo zimekuwa zikinufaika na zawadi hizi za Mheshimiwa Rais nyakati za Sikukuu mbalimbali kwa makundi maalumu.
Aidha Mhe. Mgandilwa amewataka wamiliki wa vituo mbalimbali vya kulelea Watoto waliokatika mazingira magumu kuishirikisha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa changamoto mbalimbali zinazo wakabili.
Imetayarishwa na:-
Samwel D.Mwantona
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.