Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019 Ndg. Mzee Mkongea Ally ametembelea na kukagua miradi saba ya maendeleo Wilayani Kilindi iliyonathamani ya Shilingi Bilioni 1.67, ambapo katika ukaguzi huo uliofanyika siku ya tarehe 30.06.2019 alilidhishwa na ubora wa miradi hiyo.
“Tunashukuru Mkuu wa Wilaya wataalamu wetu kwakuwa waaminifu katika mradi huu” alisema Ndg. Ally baada ya kufanya ukaguzi wa kina katika mradi wa barabara ya kutoka kijiji cha Kibirashi kwenda Kijiji cha Gombero.
Aidha katika mradi huu wa barabara viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru walilazimika kutumia vifaa vya aina mbalimbali ilikujiridhisha ubora wake, kisha wakajiridhisha kuwa ujenzi wake umezingatia viwango stahiki.
Hata hivyo Ndg. Ally ameridhishwa sana na ubora pamoja na usimamizi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa Wilayani Kilindi licha kasoro chache alizozitolea maelekezo.
Wilaya ya Kilindi imepokea Mwenge wa Uhuru tarehe 30.06.2019 katika eneo la Msente kata ya Jaila kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Vijijini. Kisha ukakagua Mradi wa Madarasa matatu ya Shule ya Wasichana Kilindi, kisha ukaweka Jiwe la Msingi katika Zahanati ya kijiji cha Kimembe na kuzindua Mradi wa Shamba la Mihogo Mpalahala kikundi cha Mwangaza na Barabara ya kutoka Kibirashi kwenda Gombero.
Mbali na miradi hiyo Mwenge wa Uhuru ulizindua Mradi wa upandaji Miti Songe wa kikundi cha Mkoba na kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji Vilindwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mhe. Sauda Mtondoo alimewapongeza wananchi kwa namna walivyoweza kuupokeaMwenge wa Uhuru kwanzia eneo la mapokezi hadi eneo la mkesha, ambapo wananchi kutoka maeneo mbalmbali waliujaza uwanja wa Mpira wa Shule ya Msingi Bokwa.
Imetayarishwa na :
Samwel D.Mwantona ( Afisa TEHAMA)
Viongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019 wakipima ubora wa Barabara ya kutoka kijiji cha Kibirashi kwenda Kijiji cha Gombero, siku ya tarehe 30.06.2019 Mwenge wa uhuru ulipotembelea Wilaya ya Kilindi. Picha na Samwel Daniel Mwantona (Afisa TEHAMA)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Mzee Mkongea Ally akisema jambo alipokuwa baada ya kukagua Mradi wa Barabara ya kijiji cha Kibirashi kwenda Kijiji cha Gombero, siku ya tarehe 30.06.2019 Mwenge wa uhuru ulipotembelea Wilaya ya Kilindi. Picha na Samwel Daniel Mwantona (Afisa TEHAMA)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Mzee Mkongea Ally akiweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Zahanati ya Kijiji cha Kimembe, siku ya tarehe 30.06.2019 Mwenge wa uhuru ulipotembelea Wilaya ya Kilindi. Picha na Samwel Daniel Mwantona (Afisa TEHAMA)
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.