• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kilindi District Council
Kilindi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara/Vitengo
      • Idara
        • Elimu Msingi
        • Elimu Sekondari
        • Afya na Ustawi wa Jamii
        • Maendeleo ya Jamii
        • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Ardhi na Maliasili
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Usafi na Mazingira
      • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Shughuli za Mifugo na Uvuvi
    • Shughuri za Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji na Umwagiliaji
    • Huduma za Kilimo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu na Majukumu yake
      • Kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao vya Kisheria
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Mradi wa Maji
      • Miradi ya Afya
    • Miradi inayoendelea
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
    • Miradi iliyokamilika
      • Huduma za Afya
      • Mradi wa Maji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video Mbalimbali

Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi yatoa Mkopo wa pikipiki 10 kwa vijana

Posted on: January 15th, 2021

Halmashauri ya wilaya Kilindi imefanikiwa kutoa mkopo wa Pikipiki 10 kwa vikundi 2 vya vijana wenye thamani ya Tsh milioni 23.5.

Akikabidhi Pikipiki hizo kwa vikundi hivyo Mh:Mbunge wa Jimbo la Kilindi Bw.Omari Kigua alisema serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Mh:Rais Dk John Pombe Magufuli imedhamiria kuwasaidia wananchi wake wakiwemo vijana kwa kutoa mikopo isiyo na riba.

Alisema mikopo inayotolewa na Halmashauri  ni kwa ajili ya vijana wote na kuongeza kuwa wanaokopeshwa wakifanya vizuri katika marejesho watatoa fursa kwa vijana wengine kupata mikopo

“Wanakilindi wote wanahaki sawa ya kupata asilimia kumi inayotokana na mapato ya wilaya Kilindi”Alisema Mh:Kigua.

Mh:Kigua pia alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi Bw.Gracian Makota  na timu yake ya wataalam kwa jitihada wanazozifanya katika kushughulikia changamoto mbalimbali za kimaendeleo zinazowakabili wanakilindi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Bw.Gracian Makota akizungumza katika makabidhiano ya Pikipiki aliwataka vijana kujikita katika sekta nyingine za uzalishaji mali kama vile useremala na kuanzisha viwanda vidogo vidogo badala ya kutegemea boda boda pekee.

Alisema fursa za kiuchumi zipo nyingi na vijana kama kundi muhimu katika kujenga uchumi wanapaswa kuzitumia fursa hizo ili waweze kujiajiri na hatimaye kufikia lengo la serikali la kuhakikisha tatizo la ajira kwa vijana linapungua.

Naye Mratibu wa dawati la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Halmashauri ya wilaya Kilindi bw.Godfrey Msuya alivitaja vikundi vilivyopatiwa Pikipiki hizo ni kutoka katika kijiji cha Kwastemba ambavyo ni Farasi na Wachakarikaji ambavyo vyote kwa pamoja vina jumla ya wanachama 20 na kuongeza kuwa kikundi cha Farasi kimepata Pikipiki 8 na Wacharikaji 2.

Alisema miongoni mwa vigezo vya kupata mkopo wa Pikipiki ni kila mwanakikindi awe amepata mafunzo ya kuendesha Pikpiki na kuwa na leseni ya udereva wa chombo hicho.

Bwana Msuya alisema katika mwaka wa fedha 2020/21 hadi sasa  Halmashauri imefanikiwa kutoa mkopo wenye thamani ya Tsh milioni 66 kwa vikundi 14,kati ya hivyo 10 ni vya wanawake,1 cha walemavu na 3 ni vya vijana.

Habari na: MODI MNGUMI-BOKWA

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILINDI MWAKA 2021 December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MHE. DC KILINDI "ZINGATIENI USAFI WA MAZINGIRA ILI KUPAMBANA NA MALARIA"

    January 16, 2021
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi yatoa Mkopo wa pikipiki 10 kwa vijana

    January 15, 2021
  • MADIWANI WATAKIWA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO

    December 18, 2020
  • Mhe.DC KILINDI ahamasisha umuhimu wa Hatimiliki Za Ardhi kwa wananchi

    December 16, 2020
  • Tazama zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda S.Mtondoo alipotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Seita
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Hati ya Mishahara
  • Mfumo wa Mpango na Bajeti
  • Mfumo wa ffars
  • Mwongozo wa Kutumia Mfumo wa FFARS
  • Taarifa kwa Umma

Tovuti Nyingine

  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Baraza la Mitihani la Taifa
  • Baraza la Taifa la Elimu ya kiufundi
  • Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora
  • Tovuti ya Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.