Jumla ya wahisiwa 406 wa ugonjwa Trachoma (Vikope) Wilayani Kilindi wamefanikiwa kuonwa na kufanyiwa uchunguzi wa macho.
Akizungumza na kamati ya uendeshaji huduma za afya wilaya Kilindi (CHMT) katika kikao kilichofanyika Halmashauri Afisa Program kutoka shirika lisilo la kiserikali la kiserikali linalojishugulisha na huduma za macho (KCCO) bwana Ndalamia Taiwap alisema wahisiwa hao walionwa katika kipindi cha kuanzia Aprili 2022 hadi Juni 2022.
Alisema katika wahisiwa hao 385 walifanyiwa uchunguzi na 21 hawakufanyiwa na kati ya waliofanyiwa uchunguzi 35 walikutwa na tatizo la vikope.
Aliendelea kusema kati ya waliokutwa na tatizo la vikope 23 walirekebishwa kope,,1 alikataa,1 alisafiri na 11 hawakuwepo nyumbani wakati zoezi la urekebishaji vikope ilinafanyika.
Bwana Taiwap alisema tatizo la Vikope(Trachoma katika wilaya Kilindi lipo na jamii hasa wanawake wamekuwa na woga wa kufanyiwa matibabu,hivyo ipo haja ya nguvu kubwa kuelekezwa katika kuelimisha jamii kukubali matibabu kwani yanaondoa tatizo la upofu unaoweza kusababishwa na Trachoma.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mganga Mkuu Wilaya Kilindi Dk Lukelemelye Mwenga alisema kamati ya CHMT itashirikisha viongozi wa jamii na wengine katika ngazi zote ili jamii iweze kufahamu kwa kina madhara ya Trachoma ugonjwa ambao umekuwa ukisababisha upofu kama muathirika hatatibiwa mapema.
Mradi wa Trachoma unaondeshwa na KCCO kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya Kilindi ulianza mwezi Agosti 2021, umefanikiwa kutoa huduma katika vijiji 87 na unatarajiwa kukamilisha vijiji 15 mwaka huu,unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba,2022.
NA MODI MNGUMI KILINDI.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.