Siku chache baada ya kuingiziwa fedha na serikali kuu kiasi Cha shilingi milioni 360 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 18 vya madarasa tayari Halmashauri ya wilaya Kilindi imeanza utekelezaji kwa kuanza kukagua maeneo ya ujenzi
Pichani juu ni timu ya ukaguzi ujenzi wa vyumba hivyo ikiongozwa na Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya Kilindi ndugu Bahati aliyevaa suti ya bluu ikifanya ukaguzi wa maeneo vyumba hivyo vitakapojengwa katika shule ya sekondari Kibirashi iliyopo kata ya Kibirashi
Ujenzi wa madarasa hayo 18 unatakiwa kutekelezwa kwa haraka ili kutatua tatizo la upungufu wa vyumba hivyo
Awali akizungumzia fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kilindi ndg Gracian Makota amesema ujenzi wa vyumba hivyo katika shule za sekondari utatekelezwa haraka iwezekanavyo na kuwata wahusika wote wa ujenzi kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza ujenzi kwa wakati
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.