Hii ni kauli unayoweza ukaisema baada ya Kamati ya Michezo Wilaya ya Kilindi kufanya Bonanza kubwa la michezo mbalimbali lililofanyika shule ya msingi Bokwa jana tarehe 30 March 2019.
Ambapo wananchi na Viongozi wote wa Serikali na Siasa wa Wilaya ya Kilindi wakiongozwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo walikutana kwa pamoja katika bonanza hilo.
Aidha ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilindi kwa kushirikia na Mkurugenzi Mtendaji wameunda kamati ya michezo ya Wilaya, yenye lengo la kusimamia Michezo mbalimbali ili kusudi kuinua vipaji lakini pia kuwaunganisha vijana na wananchi wote kwa ujumla.
Tarehe 30 Machi 2019 (jana) ni siku ambayo itabakia katika kumbukumbu za wanakilindi kutokana na michezo iliyofanyika katika bonanza hilo kuvutia wengi yaani si watoto, vijana wala wazee kila mmoja alishiriki kwa nafasi yake.
Akizungumzia bonanza hilo kwa furaha Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo alisema “Mikakati yetu kama Wilaya nikuona zoezi hili la michezo linaendelea si tu kwa wilaya mpaka ngazi ya Kijiji”
Aidha kamati hii iliyochini ya Mwenyekiti Bi.Warda Maulid (katibu tawala Wilaya ya Kilindi) imeanza kazi kwa kuratibu bonanza hili lenye mafanikio lililohusha timu kutoka katika tarafa nne za Wilaya ya Kilindi.
Moja ya michezo ilifanyika ni mpira wa miguu, mpira wa Pete, Mpira wa Mikono,Kuvuta kamba, Sarakasi, kukimbiza kuku. Michezo hii yote haikubagua umri wa jinsia kila mmoja alishiriki kwa nafasi yake.
Mpira wa Miguu fainali walicheza tarafa ya Kimbe na tarafa ya Kwekivu ambapo tarafa ya Kwekivu waliibuka washindi baada ya kupata penati nane kwa saba kutokana na dakika 90 kumalizika kwa sale ya bao moja kwa moja.
Katika hali isiyo ya kawaida licha ya mvua kunyesha wakati michezo ikiendelea lakini mamia ya washiriki waliendelea kubaki katika kiwanja kushuhudia michezo hiyo iliyoweza kuwaunganisha wanakilindi kuwa kitu Kimoja.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya alitumia jukwaa hilo kutoa elimu ya mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI, Malaria lakini pia kuwahamasisha wananchi kuhusu Uchaguzi wa Serikari za Mitaa.
Kaimu mkurugenzi wa Wilaya ya Kilindi Ndg. Edward Masona aliipongeza sana kamati kwa maandalizi mazuri lakini pia alihamasisha wananchi kwendelea kujihusisha na michezo kwakuwa kupitia michezo maadui wanaweza kukaa pamoja.
Imeandaliwa na:
Samwel D.Mwantona ( Afisa TEHAMA )
Kikundi cha Sarakasi kata ya Bokwa kikionyesha burudani wakati wa tamasha la Michezo Wilaya ya Kilindi lililofanyika Shule ya Msingi Bokwa siku ya tarehe 30 Machi 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo akikagua timu ya Tarafa ya Kwekivu walipokuwa katika bonanza la Michezo Wilaya ya Kilindi lililofanyika shule ya Msingi Bokwa tarehe 30 Machi 2019.
Katibu Tawala Wilaya ya Kilindi Bi. Warda Maulidi alipokuwa akiongoza Maandamano siku ya Bonanza la Michezo Wilaya ya Kilindi lililofanyika Shule ya Msingi Bokwa tarehe 30 Machi 2019.
Diwani wa kata ya Bokwa Mhe. Idrisa Mgaza akiwa katika maandamano ya Bonanza la Michezo Wilaya ya Kilindi, lililofanyka shule ya Msingi Bokwa siku ya tarehe 30 Machi 2019.
Baadhi ya zawadi zilizoandaliwa kwa washindi wa Bonanza la Michezo Wilaya ya Kilindi lililofanyika tarehe 30 Machi 2019 shule ya msingi Bokwa.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maandamano ya Bonanza la Michezo Wilaya ya Kilindi lililofanyika Shule ya Msingi Bokwa tarehe 30 Machi 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo akimpa hongera mshindi wa mchezo wa kukimbiza kuku wakati wa Bonanza la Michezo la Wilaya ya Kilindi lililofanyika Shule ya Msingi Bokwa tarehe 30 Machi 2019.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya kilindi Ndg. Gracian Makota akisikiliza jambo kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Kilindi Mhe. Omary Kigua walipokuwa katika Bonanza la Michezo Wilaya ya kilindi lilipofanyika shule ya Msingi Bokwa tarehe 30 Machi 2019.
Kikosi cha Askari Mgambo kikitoa burudani ya gwalide katika Bonanza la Michezo Wilaya ya Kilindi lililofanyika Shule ya Msingi Bokwa tarehe 30 Machi 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo akizungumza na wananchi waliojitokeza katika Bonanza la Michezo Wilaya ya Kilindi, lililofanyika shule ya Msingi Bokwa tarehe 30 Machi 2019.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.