Wakazi wilayani Kilindi wametakiwa kujiandaa kutumia fursa za mradi wa bomba la Mafuta pindi mradi huo utakapoanza utekelezaji wake .
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya Kilindi Mh:Abel Yeji Busalama wakati alipokuwa akifungua mafunzo kuhusu ujenzi wa bomba hilo yaliyofanyika mjini Songe.
Alisema jukumu la wadau na wananchi wote ni kuhakikisha mradi unafanikiwa,unakuwa salama wananchi wanauelewa na kujua faida zake kwa maendeleo ya jamii inayopitiwa na mradi huu.
“Ili kuhakikisha mradi unafanikiwa katika utekelezaji wake wananchi wote na sisi wote jukumu letu ni kuupenda mradi na kujua faida zake”Alisema Mh:Busalama
Awali akitoa taarifa ya mambo mbalimbali yaliyotekelezwa kabla ya kuanza ujenzi wa mradi bwana Asiadi Mrutu Mratibu wa mradi wa mafuta salisema jumla ya Tsh milioni 123 zimelipwa kama fidia kwa wakazi wa mkoa wa Tanga ambao maeneo yao yatapitiwa na bomba hilo.
Alisema sanjari na hilo tayari mikataba mbalimbali imeshasainiwa ikiwemo mkataba hodhi na mkataba wa ardhi na kuongeza kuwa wakazi wa mkoa wa Tanga wanatakiwa kuzitumia fursa za mradi kwa ajili ya maendeleo yao na taifa.
Mradi wa bomba la mafuta katika wilaya Kilindi utapita katika kata za Kibirashi,Saunyi,Kisangasa,Mabalanga na Mkindi na utakuwa na urefu wa kilometa 66.6.
MODI MNGUMI.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.