Wajasiriamali wadogo wilayani Kilindi wamepataiwa vitambulisho vya utambuzi kwa lengo la kuwaondolea kero mbalimbali ambazo wamekuwa wakikumbana nazo katika shughuli zao.
Viyambulisho hivyo vimetolewa na Mkuu wa wilaya Kilindi Mh:Sauda Mtondoo katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kilindi na kuhuduhuriwa na wajasiriamalai wadogo wa kata za Bokwa na Songe na baadhi ya viongozi wa taasisi za umma wilayani hapa.
Alisema wajasiriamali wadogo wamekuwa wakifanya shughuli zao katika hali ya usumbufu na serikali imeliona hilo na kaumua kuwapatia vitambulisho maalum vya utambuzi na kwamba hakuna mtu yeyote anaepaswa kuwasumbua.
Mh:Mtondoo alisema utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho linapaswa liende kwa uadilifu kwa wajasiriamali wadogo wenyewe kutoa taairfa sahihi ambazo zitasaidia kuboresha zoezi hilo na kuwanufaisha wale ambao wana sifa stahiki kwa mujibu wa vigezo vinavyotakiwa.
“Vitambulisho hivi haiviuzwi vinatolewa ili wajasiriamali wadogo waweze kufanya kazi zao kwa amani bila kero“ alisema Mh:Mkuu wa Wilaya na kuongeza kuwa kiasi cha Tsh 20,000/= wanazotoa wajasiriamali hao kwa mwaka ni gharama za kutengeneza vitambulisho hivyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Meneja Mamalaka ya Mapato(TRA) Wilaya Kilindi bwana Enos Viji alisema vitambulisho ni chachu ya maendeleo katika kukuza uchumi wa nchi na kuwataka wajasiriamali wadogo kutumia vizuri fursa hiyo muhimu iliyotolewa na serikali
Alivitaja vigezo ambavyo wajasiriamali wanaopaswa kupatiwa vitambulisho kuwa ni mjasiriamali awe na mauzo ghafi yasiyozidi shilingi milioni nne kwa mwaka,awe hajawahi kusajiliwa na Mamlaka ya Mapato(TRA) na kupewa Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN),ajaze fomu maalum kama Mfanyabiashara wa Sekta isiyo rasmi na atalipa shilingi elfu ishirini kwa mwaka.
Zoezi la ugawaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo lilioanza katika kata za Songe na Bokwa litaendelea katika kata niyngine 19 zilizobaki.
Na Modi Mngumi
MWISHO.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.