Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh:Martine Shigela amewataka wachimbaji na wanunuzi wa madini kuanza mchakato wa kuwa na benki yao ili kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.
Mkuu wa mkoa ametoa ushauri huo wakati wa akizindua soko la madini wilayani Kilindi
Amesema wachimbaji hasa wadogo wadogo wanakabiliwa na changamoto nyingi na kubwa ni ukosefu wa mitaji ya kutosha kwa ajili ya kazi wanayoifanya.
Amesema benki hiyo itakuwa ni muhimu kwa ajili ya kuwasaidia wachmbaji na wanunuzi wa madini na kuwawezesha kuwa na uhakika wa mitaji.
Mh:Mkuu wa mkoa pia amezitaka taasisi nyingine za kibenki kuona uwepo wa madini ni fursa katika wilaya Kilindi hivyo na kuona umuhimu wa kuwekeza na kuongeza kuwa serikali itaimarisha ushirikiano na ulinzi kwa wadau wa sekta ya madini.
Amesema uwepo wa soko la madini ni utekelezaji kwa vitendo maagizo ya Mh:Rais John Pombe Magufuli na kwamba jitihada hizi zitasaidia kuongeza mapato ya wachimbaji na serikali.
Mkuu wa mkoa ameongeza kusema kuwa kuwepo kwa soko kunatikiwa kwenda sanjari na kuongezeka kasi ya uwepo wa madini na ununuzi na kuongeza kuwa baada ya kuwepo soko hili yeyote atakayefanya biashara ya madini nje ya soko ni sawa na mhujumu wa uchumi.
Awali akitoa taarifa fupi ya madini Mkuu wa wilaya Kilindi Mh:Sauda Mtondoo amesema soko hilo lilianza tarehe 23/07/2019 na hadi uzinduzi wake zaidi ya Kg 19 zimeuzwa na kuzitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wachimbaji madini kuwa ni uelewa mdogo wa masoko ya madini yanavyoweza kuwasaidia na upatinaji wa leseni.
Wakielezea baadhi ya matatizo/changamoto zinazowakabili wachimbaji wa madini ni ukosefu wa umeme ambayo ni nishati muhimu kwa ajili ya kuendeshea shughuli za uchimbaji .
Habari Na:Modi Mngumi
Afisa Habari-Kilindi
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.