Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kilindi Ndg.Gracian Max Makota, amewataka wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata kuhakikisha kuwa wanatenda haki kwa vyama vya siasa na wagombea wote watakao jitokeza kushiriki katika Uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28.10.2020.
Ndg. Makota ameyasema hayo leo tarehe 07.08.2020 alipokuwa akitoa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata, mafunzo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi.
“Jiepusheni na kufanya kazi kwa mazoea” alisema Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kilindi Ndg.Gracian Max Makota alipokuwa akitoa mafunzo.
Aidha msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kibirashi Bi. Mwanaisha Sendege alitoa shukrani kwa wawezeshaji wa mafunzo, lakini pia aliwahimiza wasimamizi wenzake kuhakikisha wanafuata sheria, taratibuna kanuni pamoja na miongozo iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Mwaka 2020.
Mafunzo haya yaliyolenga kuwajengea uwezo wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata yatahitimishwa siku ya jumapili ya tarehe 09.08.2020.
Habari hii imeandaliwa na :
Samwel Daniel Mwantona
Afisa TEHAMA
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.