Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi Ndg.Clemence Mwakasendo, akipanda mti wa kivuli siku ya kilele cha maadhimisho ya Juma la kupanda miti kiwilaya kwenye eneo la shule ya msingi Makingo iliyopo kata ya Kisangasa.
Sambamba na kushiriki kwenye zoezi la upandaji miti siku ya kilele cha Juma la kupanda miti kiwilaya, Mkurugenzi Mtendaji alitembelea jengo la darasa moja lililojengwa na wananchi wa kijiji cha Makingo na kuahidi kulifanyia ukarabati kwa kutoa saruji, misumari na gharama nyingine kwenye bajeti mpya itakayo anza kutekelezwa mwaka wa fedha 2017/18.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.