Mnyama adimu na mwenye mvuto, Kakakuona ameonekana katika kijiji cha Kilwa kata ya Kilwa ndani ya Wilaya ya Kilindi mnamo tarehe 14/03/2019.
Mnyama huyu ni miongoni mwa wanyama adimu na waliojizolea umaarufu mkubwa kote ulimwenguni kwa tabia yake ya kutabiri mambo mbalimbali kwa kuchagua kitu kimoja wapo kati ya vitu mbalimbali vilivyowekwa mbele yake.
Aidha Wilaya ya Kilindi imekuwa miongoni mwa wilaya chache nchini Tanzania zilizopata bahati ya kumona mnyama huyu kwa miaka miwili mfululizo. Ambapo kwa mara ya kwanza alionekana katika Kitongoji cha Matangagoja kilichopo kijiji cha Kilindi Asilia ndani ya kata ya Kilindi mwaka 2018 mwezi wa saba.
Hata hivyo alipooneka kwa mara ya kwanza katika kijiji cha Kilindi Asilia wanakijiji walimwekea mahindi, fedha na maguzi ilikubaini utabiri wake kwa maeneo yao na Wilaya kwa ujumla. Aidha mnyama huyu alielekea kwenye maguzi badala ya fedha na mahindi.
Akielezea tukio hilo Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Kilindi Ndg.Ramadhani Athumani Msuluwa alisema “ Utabiri wa Kakakuona ulikuwa sahihi kwasababu msimu ule hatukupata mazao ya kutosha kutokana na mvua kubwa iliyoharibu mazao”.
Kwa awamu hii ya pili alipoonekana ndani ya kijiji cha Kilwa hakuweza kufanya utabiri wowote. Ila wananchi waliopata fursa ya kumtizama walivutiwa sana na kuitizama Wilaya ya Kilindi kuwa ni eneo lenye bahati kubwa ndani ya Tanzania kwa kupatikana mnyama huyo kwa miaka miwili mfululizo.
Lakini pia Ofisi ya Mkurugezi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kituo cha Kwediboma imekamilisha taratibu zote na kumkabidhi Mhifadhi wa wanyama pori wa Mbuga ya Sadani iliyopo Wilaya ya Pangani Mkoa wa Tanga mnamo tarehe 21/03/2019
Hii ni mara ya pili Mkurugenzi Mtendaji kufanya utaratibu huu wa kuwakabidhi wanyama pori hawa katika hifadhi ya Sadani baada ya kumkabidhi Kakakuona aliyepatikana Kijiji cha Kilindi asilia Kwa Wahifadhi hao mnamo tarehe 31/07/2019. Ikiwa ni lengo la kutunza wanyama hawa kwa vizazi vijavyo vya Taifa letu.
Kakakuona ni mnyama aliyezungukwa na magamba makubwa katika sehemu ya mwili wake hari ambayo utoa wakati mgumu kwa maadui kumshambulia kutokana na ugumu wa magamba hayo hasa pale anapojivilinga aisipo maadui.
Imeandaliwa na.
Samwel D.Mwantona (Afisa TEHAMA)
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.