Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe.Sauda Mtondoo amekabidhi pikipiki nane kwa vikundi vitatu vya vijana zilizonunuliwa na Halmashauri kwaajili ya kutoa ajira kwa vikundi vya vijana leo tarehe 21/03/2019, alipokuwa katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Halmashauri.
“ Tunawakabidhi pikpiki hizi mwende mkafanyie kazi lakini pia mzitunze ” alisema Mhe.Mtondoo alipokuwa akikabidhi pikipiki hizo kwa vijana, lakini pia amewahasa kuhakikisha wanarejesha fedha kwa wakati ili Halmashauri izitumie fedha hizo kuwakopesha vijana wengine.
Hata hivyo mwakilishi wa vijana hao waliopatiwa mkopo wa pikipiki hizo Ndg. Kisailo Muya Kisailo, alitoa shukrani kwa Halmashauri kulingana na mkopo huo, lakini pia ameahidi kufanya kazi kwa juhudi ili kuweza kurejesha mikopo hiyo kwa manufaa ya vijana wengine.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Gracia Makota kwa kipindi cha miezi nane mpaka sasa imekwisha kutoa Mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni 88.93 kwa makundi ya wanawake, Vijana na Walemavu .
Kwa upande wa wanawake Halmashauri imetoa jumla ya shilingi milioni 42 katika kuwawezesha wanawake kwenye miradi mbalimbali waliyoiandaa ili kuweza kujikwamua kimaisha. Lakini pia kwa vijana Halmashauri imekwisha toa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 42.13
Mbali na makundi hayo Kundi la walemavu nalo limepewa mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni 4.8. Hizi fedha zote zilizotolewa kwamakundi haya zimetokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Naye Afisa Vijana wa Wilaya ya Kilindi Ndg. Godfrey Msuya amehitaji makundi haya muhimu kuchukua hatua ya kuunda vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kunufaika na mikopo inayotolewa na Halmashauri. Aidha Ofisi ya Mkurugenzi kwa kusimamia hilo imekuwa ikiendelea kusajili na kupokea miradi ya Vikundi mbalimbali ili kuweza kuvisaidia kufanikisha na kujikwamua kiuchumi .
Hata hivyo Mhe. Mtondoo leo ameendelea kupokea kupokea mabati 184 kutoka kwa wadau mbalimbali wamaendeleo. Miongoni mwa mabati hayo mabati 84 yametolewa na Benki ya Mwalimu Tanzania kwa lengo kusaidia kuezeka maboma ya shule za Sekondari ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019.
Akipokea bati hizo Mkuu wa Wilaya ameendelea kuwaomba wadau wa maendeleo kuendelea kutoa misaada ya hali na mali katika kuboresha miundombinu ya Elimu kwalengo la kutatua changemoto zinazoikabili sekta muhimu ya Elimu Wilayani Kilindi.
Imeandaliwa na.
Samwel D.Mwantona ( Afisa TEHAMA)
Afisa wa Kitengo cha ukuzaji Biashara na Masoko benki ya Mwalimu Ndg.Moris John (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo moja kati ya mabati 84 yaliyotolewa na benki ya Mwalimu kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa wilayani Kilindi. Makabidhiano hayo yamefanyika katika hafla fupi iliyofanyika Ukumbi mdogo wa halmashauri ya Wilaya ya Kilindi leo tarehe 21/03/2019. Picha na Samwel D.Mwantona (Afisa TEHAMA)
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe.Sauda Mtondoo akiendesha moja ya pikipiki zilizotolewa kwa vikundi vya vijana wajasiriamali Wilayani Kilindi. Alipokuwa katika hafla fupi iliyofanyika Katika ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Kilindi le oleo tarehe 21/03/2019. Zilizoandaliwa kwaajili ya kukabidhi pikipiki hizo kwa vijana hao. Picha na Samwel D.Mwantona (Afisa TEHAMA)
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo (Kulia) akimkabidhi Ndg. Kisailo Muya Kisailo ufunguo wa pikipiki alipokuwa katika hafla ya kukabidhi pikipiki nane kwa vikundi vitatu vya vijana wajasiriamali Wilayani Kilindi. Hafla hii imefanyika Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Kilindi leo tarehe 21/03/2019. Picha na Samwel D.Mwantona (Afisa TEHAMA)
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.