Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo amewataka viongozi katika ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji kuhakikisha wanasajili kaya zote katika maeneo yao ili wakati wa zoezi la ugawaji wa vyandarua kila kaya iweze kunufaika na kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria, ameyasema haya alipokuwa akifungua mafunzo Ukumbi wa Halmashauri
Mhe. Mtondoo ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya usajili wa kaya na ugawaji wa vyandarua kwa wawezeshaji wa Wilaya ya Kilindi jana tarehe 23.07.2020. Baada ya mafunzo hayo wataalam hao watatoa mafunzo katika ngazi ya vijiji na kata Wilaya ya Kilindi.
Hivyo wananchi wote mnahimizwa kujitokeza katika zoezi la usajili linalotazamiwa kuanza mapema wiki ijayo kwani watakao nufaika na zoezi la vyandarua hivyo ni wale tu walijiandikisha.
Aidha mafunzo haya kwa Viongozi wa Wilayani yametolewa na watalaam kutoka wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na OR-TAMISEMI kwa muda wa siku moja.
Habari hii imeandaliwa na :
Samwel Daniel Mwantona
Afisa TEHAMA
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.