Mkuu wa Wilaya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo amezitaka kamati zinazoendesha majosho Wilayani Kilindi kutoa taarifa za mapato na matumizi katika mikutano mikuu ya Serikali za vijiji, alipokuwa akizindua kampeni ya kuogesha mifugo leo tarehe 25 Feb 2019 katika kijiji cha Kibirashi kata ya Kibirashi.
Mhe. Mtondoo ameyasema hayo alipokuwa akizindua kampeni ya uogeshaji mifugo ndani ya Wilaya ya Kilindi kwa wafugaji wa Kata ya Kibirashi kijiji cha Kibirashi leo tarehe 23 Feb 2019.
“Sisi kama kamati ni sehemu ya Serikali, tunafanya kazi kuisaidia Serikali ,hivyo mrejesho ni kitu muhimu” Aliyasema hayo Mhe. Sauda Mtondoo alipokuwa akizungumza na wafugaji wa kijiji cha Kibirashi. Akizungumza hayo amekemea tabia ya viongozi wa majosho kusahau wajibu wao kwa wafugaji na wanakijiji.
Aidha amezitaka kamati hizo na wafugaji kuhamasishana kuhakikisha kuwa kila mfugaji anakuwa na tabia ya kuogesha mifugo katika mojosho yaliyo karibu kwani hii itasaidia kuikinga mifugo yao dhidi ya magonjwa yanayoshambulia mifugo, lakini pia kuwa chanzo cha mapato katika kijiji.
Kampeni hii imezinduliwa baada ya Serikali kutoa Ruzuku ya dawa zinazotumika kuosha mifugo katika majosho jumla ya lita 60.25 kwa Wilaya ya Kilindi hali iliyopokelewa kwa Furaha kwa wafugaji Wilayani kilindi.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Josho la Kijiji cha kibirashi Ndg. Mkande Mndiga ameishukuru Serikari kwakutoa dawa ya Ruzuku kwakuwa kupitia josho magonjwa yanayoshambulia mifugo yatadhibitiwa
Naye kaimu Afisa Mifugo Wilaya ya Kilindi Daktari Emmanuel Towwo amezitaka kamati za Majosho kwa kushirikiana na Wafugaji kuunda sheria ndogo zitakazo hakikisha wafugaji wanaogesha mifugo yao katika majosho ili kuweza kuyaendesha majosho hayo lakini pia kudhibiti magonjwa yanayoshambulia mifugo.
Imeandaliwa na.
Samwel D.Mwantona (Afisa TEHAMA)
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo akimimina dawa katika shimo la maji yanayotumika kuogeshea Mifugo katika Josho, alipokuwa akizindua kampeni ya kuogesha Mifugo Kijiji cha Kibirashi Kata ya Kibirashi tarehe 26 Feb 2019
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo akikagua zoezi la kuingiza mifugo katika Josho muda mfupi baada ya kuzindua Kampeni ya kuogesha Mifugo kijiji cha Kibirashi Kata ya Kibirashi tarehe 26 Feb 2019.
Mifugo ikiwa eneo la kuingilia ndani ya Josho tayari kwa zoezi la kuogeshwa mara baada ya ufunguzi wa kampeni Uogeshwaji Mifugo Wilaya ya Kilindi katika kijiji cha Kibirashi tarehe 26 Feb 2019
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.