Mkuu wa Wilaya ya kilindi Mhe. Sauda S.Mtondoo leo tarehe 22.05.2019 ametangaza rasmi kuondoa zuio la usafirishaji mazao nje ya Wilaya ya Kilindi. Kwani mnamo tarehe 08.05.2019 kwenye Baraza la Madiwani Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi alitangaza zuio la wafanyabiashara kusafirisha mazao nje ya Wilaya kutokana na hali ya mvua kwa wakati huo kutokuwa ya kuridhisha.
Hivyo kutokana na mvua zilizonyesha kwa kipindi hiki Mhe. Sauda Mtondoo ametangaza Rasmi kusitisha zuio hilo, lakini pia kuwasihi wakulima/wananchi kuuza mazao ambayo ni ziada tu.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.