Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mhe. Sauda Mtondoo anawaalika wananchi wote ndani na nje ya Wilaya kushiriki shamrashamra za mbio za Mwenge zitakazo ambatana na kuzindua Miradi mbalimbali iliyotekelezwa.
Mwenge wa Uhuru tunatarajia kuupokea siku ya Tarehe 07/10/2018 katika Viwanja vya shule ya Msingi Kolang’a Kata ya Jaila Kuanzia majira ya saa 1:00 asubuhi hivyo Wananchi wote mnaombwa kufika mapema kabla ya saa 1:00 asubihi.
Msafara wa Mwenge utaanzia Shule ya Msingi Kolang’a kwenda Mradi wa Ufugaji Nyuki na Utunzaji wa Mazingira Kijiji cha Mkindi, Uzinduzi wa Vyumba Vitatu vya Madarasa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilindi, Mradi wa Zahanati ya Kijiji cha Mnkonde, Mradi wa Maji ya Bomba Vijiji vya Muungano na Kigwama, Uzinduzi wa Barabara ya Kimembe Kilwa Km 3.3. na Mkesha utafanyika katika kiwanya ya makasini-Kwediboma.
Hivyo mkuu wa Wilaya anawaalika Wananchi wote kukusanyika katika maeneo yatakayo pitiwa na Mwenge wa Uhuru lakini bila kukosa eneo la Mkesha viwanja vya Makasini –Kwediboma kuanzia saa 7:00 mchana.
Copyright ©2018 Kilindi DC . All rights reserved.